Tuesday, 13 July 2021

ununuzi wa vipakatalishi kugharimu mlipa ushuru Sh105 milioni

 

KAMATI ya Bunge kuhusu Utangazaji na Maktaba sasa inapendekeza kuwa wabunge wote 349 wanunuliwe vipakatalishi za matumizi katika mikutano yao kupitia mitandaoni.

Kamati hiyo inapendekeza kwamba wabunge wanunuliwa aina ya kisasa ya laputopu kwa jina Apple MacBook Pro, ambayo inaweza kugharimu hadi Sh105,000 kila moja.

Hii ina maana kuwa ikiwa mapendekezo hayo yataidhinishwa na wabunge, ununuzi wa mitambo hiyo utamgharimu mlipa ushuru Sh105 milioni ikizingatiwa kamati hiyo inapendekeza Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi pia anunuliwe kipakatalishi cha aina hiyo.

Photo:Courtesy
Huenda mlipa ushuru akagharimika zaidi ikiwa maseneta 68 pia watapendekeza wanunuliwe vipakatalishi kwa gharama ya mlipa ushuru.

Ripoti hiyo ya kamati ya Utangazaji iliyowasilishwa bungeni wiki jana, ilisema kuwa wabunge wanapendelea kutumia vipakatalishi katika mikutano yao ya mtandaoni badala ya iPad.




No comments:

Post a Comment