Saturday 4th April 2026
Edwine Ochaly
South West Nyanza Field limezindua rasmi Kituo cha Rabwao wakati wa ibada ya Sabato iliyofanyika kwa shamrashamra katika Shule ya Sekondari ya Rabwao, iliyoko Wodi ya Muhuru, Kaunti Ndogo ya Nyatike.
Hafla hiyo iliongozwa na Rais Mathews Kwasi, na iliwaleta pamoja makanisa 28 ambayo sasa yatakuwa sehemu ya kituo kipya kilichoanzishwa. Kituo hicho kitaongozwa na Mchungaji Enos Okomo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Profesa Rose Ogwang Odhiambo, aliyewakilisha Serikali ya Kaunti ya Migori, aliwasilisha salamu kutoka kwa Mheshimiwa Gavana Dkt. Ochilo Ayacko. Aliwapongeza viongozi wa kanisa pamoja na waumini kwa kufikia hatua hii muhimu, na kuwahakikishia ushirikiano na msaada endelevu kutoka kwa Gavana katika kukuza maendeleo ya jamii na mshikamano wa kijamii.
Uzinduzi huu unaashiria hatua muhimu katika kuimarisha umoja wa kidini na utoaji huduma ndani ya eneo hili la Muhuru Bay na vitongoji vyake.
Ukumbukwe kwamba pia ilikuwa ni siku muhimu ya kusherehekea miaka 100 tangu dhehebu la Waadventista wasabato iliooingia eneo hili mwaka wa 1926.
Hadi kufikia sasa , wachungaji 59 wameweza kuhudumu katika kituo hiki mpya, huku mtaa wa Rabwao imeweza kuongozwa na wachungaji thelathini na wawili, Obolo ishirini, Senye 4, Muhuru Central 2 na Lwanda 1.
Wanasema wanamalengo ya kufungua kituo cha uchapishaji ambayo gharama yake ni Shilingi Laki Saba na arubaini. Huku wakikuza nyoyo za washiriki.
Kwa sasa mitaa yote tano inaongozwa na Wachungaji Enos Okomo -Rabwao, Caleb Ligawa-Obolo, Isaac kogah- Muhuru Central, Kennedy Adiang - Senye na Paul Wariga- Lwanda.












.jpg)





















